Help
Change language Swahili (Kiswahili)

Jinsi ya kuwa mwanachama

New: Corylus jacquemontii Shop (India), Mimea kudumu, Matunguu

Become a KPR member, and enjoy cheaper prices immediately. Register here.

Fomu ya usajili uwanachama

Napenda kuwa Mwanachama wa KPR

Taarifa za uwanachama

Kuanzia 2007 unaweza kuwa Mwanachama wa KPR hata kama huwezi kuzungumza au kuelewa lugha ya Kislovak.
Mwaka 2000, tulianzisha Klabu yetu kwa lugha ya Kislovak. Tangu hapo kumekuwa na wanachama wengi waliojiunga hasa kutoka Slovakia na Ucheki.
Sasa unaweza kufurahia faida zote za uwanachama KPR Slovakia pia - na haijalishi wewe ni nani au lugha gani unazungumza.
Tunakaribisha mtu yeyote kutoka kokote duniani ambaye anapenda mimea. Jiunge nasi sasa!
Kwa bahati mbaya, harasa moja bado inaendelea kuwepo. Hutaweza kusoma jarida letu la klabu la Botanix, kama huwezi kuelewa lugha yoyote kati ya zilizomo kwenye Botanix.
Kwa upande mwingine, kwanini usianzishe jarida lako kwa lugha yako? Ungana na walima wengine wa bustani, mnaozungumza lugha sawa, na anza kuandika au kukusanya habari zinazovutia kuhusu bustani, mimea nk kisha anza na Botanix yako mwenyewe kwa lugha yako!
Hakuna vizuizi kwa kujikamilisha mwenyewe!
Kwa upande mwingine, taarifa za ukuzaji ni maalumu kwa wakulima wa bustani wa Slovak, haziwezi wakati wote kutumika kwenye maeneo ya tropika na kinyume chake, hivyo mabadiliko ya lugha ya asili ya Botanix yangefaa.

Uwanachama wa KPR Slovakia

Kwanini uwe Mwanachama wa KPR

1. Wanachama wa KPR wanaweza kuweka oda zao kwa bei nzuri . angalia baadhi ya mifano hapo chini. (Hakuna kikomo kwa oda.)

Bei kwa Wanachama wa KPR Bei kwa wasio Wanachama % punguzo
0,50 € 0,70 € 29%
0,70 € 0,90 € 22%
1,00 € 1,50 € 33%
3 € 4 € 25%

2. Kila Mwanachama anaweza kuchukua mbegu 5 za bure za sampuli kila mwaka (isipokuwa mbegu za michikichi, cycads na mbegu za baadhi ya spishi zilizochaguliwa) kutoka kwenye Benki ya Mbegu na Mimea ya KPR. Wanachama wanapatiwa punguzo la 50% kwa sampuli zingine (bei ya kawaida ni Euro 1 kwa sampuli; wakati bei kwa wanachama wa KPR ni Euro 0.50 tu).

3. Oda za wanachama wa KPR zinashughulikiwa kabla ya oda za wasio wanachama.

4. Ushauri wa bure katika lugha 11 kwa mwaka kuhusu ukuzaji wa mimea.

5. Unaweza kutumia huduma za Akaunti ya Wazi.

Akaunti ya wazi - Taarifa kuhusu Akaunti ya Wazi
Akaunti ya wazi ni njia nzuri ya kununua bidhaa KPR. Unatuma pesa kwetu kabla ya kuweka oda - wakati wowote unapotaka kuweka oda, oda yako itatozwa kupitia salio lako la pesa lililopo kwenye akaunti yako haraka. Hii ina maana kwamba hatuhitajiki kusubiri hadi tupokee malipo yako kabla ya kuanza oda yako, na oda yako inaweza kufungashwa na kusafirishwa haraka. Unaweza kuongeza fedha kwenye akaunti yako ya wazi, kwa kutumia njia zozote za malipo zinazokubalika.
Wakati wowote unapotaka kuongeza fedha kwenye akaunti yako, andika namba yako binafsi ili nasi tuweze kubaini dhumuni la malipo yako. Tunaweza kuongeza fedha kwenye akaunti yako ya wazi mara tu tutakapo pokea malio yako. Hakuna ukomo wa kuongeza fedha kwenye Akaunti yako ya Wazi. Salio lililopo kwenye Akaunti ya wazi unaweza kulitumia mara tu fedha zinapoongezwa.
Kana unapenda kulipia oda yako kwa kutumia Akaunti yako ya Wazi, tujulishe kwa ujumbe ufuatao: “oda yangu italipwa kwa kutumia Akaunti yangu ya Wazi namba XXXXXXX” oda yako itatozwa mara tu itakapoanza kushughulikiwa na itatumwa mara tu itakapofungashwa.
Unaweza kudai fedha kutoka kwenye Akaunti yako ya wazi urudishiwe. Hata hivyo ukumbuke kwamba utatozwa ada kwa kurudishiwa fedha. Hakuna ada kama utarudishiwa fedha zako kwa kupitia PayPal, na kiwango kikubwa cha ada kwa kurudishiwa fedha zako kupitia moneybookers.com ni Euro 0.50. hakuna ada yoyote iwapo fedha zako zitarudishwa kwa kuhamisha kupitia benki ndani ya Slovakia na Chekia. Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa ada inayotakiwa au njia nyingine za malipo kwa nchi yoyote ile. Tutarudisha fedha zako kutoka kwenye Akaunti yako ya Wazi ndani ya siku 60 baada ya ombi lako kupokelewa.
Zingatia: kwa kutumia Akaunti ya Wazi kutaokoa pesa zako kwenye ada za kuhamisha pesa. Unatakiwa kuhamisha fedha zako mara moja tu kwenye Akaunti yako ya Wazi na kulipia oda zako kutoka kwenye akaunti hii mara nyingi upendavyo.
Maswali yoyote?

6. Kama oda zako kwa mwaka 2010 ni za zaidi ya Euro 80, unaweza kuweka oda ya mbegu au mimea hadi zenye thamani ya Euro 10 bila gharama zozote!

7. Tiketi ya bahati nasibu ya mwaka zenye bei ya Euro 50, 30, na 15 kufanya manunuzi bure!

...na faida nyingine nyingi ambazo tutaendelea kukupa taarifa.

Masharti ya uwanachama

1. Unahitajika kujaza Fomu ya Usajli uwanachama na kulipa ada ya mwaka ya Euro 10 kabla ya Mei 31 ya mwaka wa uwanachama. Fedha za mchango wa uwanachama zinatumika kwa maendeleo ya shughuli za KPR kote ulimwenguni.

Ada ya mwaka ya uwanachama kwa mwaka 2010

(uwanchama ni hai kuanzia 1.10.2009 hadi 31.12.2010)

Mchango wa mwaka Mwaka wa kwanza Kurudia tena kwa mwaka ujao
10 Euro 5 Euro

2. Unatakiwa kuweka angalau oda 2 kwa mwaka kutoka kwenye bidhaa za Klabu. Hakuna kima cha chini cha ukomo kwa oda yoyote.

3. Unaweza pia kulipia ada ya kujitolea pamoja na wanachama wengine, ambayo pia itatumika kwa maendeleo ya mtandao wa KPR ulimwenguni.

Umevutiwa kuwa Mwanachama wa KPR? Ni rahisi! Jiunge nasi sasa hivi, jaza Fomu ya Usajili Uwanachama.

Fomu ya usajili uwanachama

Napenda kuwa Mwanachama wa KPR

Umeongeza kitu hiki kwenye toroli lako.